Thursday, September 14, 2006

A homegrown bug bit me

Ebu nione kama bado naweza kuandika kiswahili asili. Sijaandika kiswahili kwa miaka kadha wa khada. Natumaini haitakuwa ngumu hivyo. Ningetaka kusema mengi lakini kwa sasa nitaandika juu ya roho yangu inavyolia kila siku. Ndio, mimi ni mchovu. Sababu ya uchovu wangu ni masikitiko inayonishika kila nikifikiria kwetu;pwani. Majirani wetu akina dida na uncle hubesh, kadindo, sambaba, faiz, sofia na latifa. Kila nikitembe njee kusalimiwa na jina langu. Siku za ramadhan kupelekeana chakula kisha sahani yako inaregeshwa na chakula ya jirani yako. Asubuhi na mapema Mzee Ali akigonga dirisha la nyumba kumamusha buda kwa sababu salatul fajr iko karibu. Mwadhini wasikia kila mara na hata si moja pekee. Mskiti, leso, taraweh, udi, qasida, mshakiki......ramadhan si kamili bila vitu hivyo. Ukitoka shule, AsemaNaye yupo nje akiuza victoria na maembe za pilipili. Au kama hutaki matunda waweza kukula kachiri, mahindi, muhogo, viazi vya urojo, viazi vya pili, kaymati, mbaazi, mabuyu ama hachari . Majioni mengi tukienda lighthouse kubarizi hewa. Arusi za kiswahili na kucheza chakacha kwa mviringo. Ah! jemeni. Nitaenda nyumbani siku gani?

Mwembe tayari, makadara, blue room, steers, nyali, mamba, mombasa beach, bamburi beach bado mpo? Ama kutokuwepo kwangu imekubadilisha. Hussein bakery, nilivyopenda kununua biskuti zako kila jumapili baada ya kutoka kuogelea kwa bahari. Kila jumamosi, kuenda dil bahar kununua chicken tikka na mkate mayai. Aisee chakula si kutu peke nichohisi, lakini harufu za chukula ndio unakumbuka. Kisha nikakuwacha pwani wangu. Mpenzi wangu.

Nilisafiri kuenda Nai. Kule naye nilianza na manumba 9. Kusikia muziki na kupewa sare. Nikapata paka wangu, KCI. Nilimpata akiwa mtoto. Alinichukia kwa sababu alikuwa anamtaka mamake, lakini nilimlaza nami kwa kitanda changu. Nilimpa maziwa na vidole vyangu mpaka akawa kama mtoto wangu. Kila siku nilipotoka shule alikuwa barazani akiningojea. Akinifwata kila pahali naenda. Kisha akawa dume wa kijiji. Mapaka wa kike walijaa kwa baraza na ukuta zetu wakimlilia. Nakumbuka nikirusha kiatu changu baada ya kutoshindwa kulala usiku nzima. KCI, uko wapi sasa?

Lazima, mola akinibariki, niregea 2007. Lazima!!

9 comments:

NATIVE said...

Naomba Mola akubariki....inshaAllah utaregea nyumbani 2007.

If its any comfort roho yangu inalia with yours

By the way...unaeza kuandika kiswahili asili...u aint a hopless case like me..loool

Poundy said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Poundy said...

Nakupa vipawa hadhi yangu ikiwa nataka utuwe popote moyo wako unaoupenda.Naona nyoyo za burudika na kumbukumbu za nyumbani.Heko kwako dada kwathamani kurudi nyumbani.Kwa hakika mimi pia natarajia kwenda Kenya na Somaliamwisho wa mwaka huu au mwaka ijao januari.

PS Good to see your blog still blazing sister.I become the bigest anti-computer lately.I found adventure in the nature trails lately....


AKA Stoic

TheAdvocates said...

what can i say...i am just happy that i can find someone who can remind me of the good old days of care-free laddishness. The Maembe pilipili, mabuyu which my sisters and cousins use to consume - I have never thought hearing that would make me happier - but now they do. Those days ...highly cherished childhood in a land of immense beauty! I am even feeling more home-sick than before.

SD, walahi umenikumbusha maisha yale yanaojaza rohoni na furaha. Asante sister.

Thanks again.."tear on his eyes"

;)

SleepDepraved said...

Native, my kiswa is preschool compared to mr stoic. Sometimes I think he still lives in Kenya and writes Inshas everyday.

Stoic, its nice to get away from the computers once in a while. Just don't completely drop off plus with the winter coming those nature trails will get iced over.

Thetwoadvocates, lmao don't cry. I was arguing with my cuz the other day cause his wife came back from kenya and she brought mabuyu. It came to our house but I didn't even see one bit. The lil rugrats consumed it with a quickness. My cuz told me to stop whining and just go back to Kenya. I would too except there isn't anyone left except my grandma and charo. My friend is going back this year, so maybe I will use her as an excuse and tag along.

Hope Faith Love Happiness Adversity said...

Ala Sleep Deprived abaayo walahi you took me back to childhood memories with your MABUYU word. I am actually salivating due to you. Mabuyu with chilli. I have to call my sister and try to have her send me some. Famous Baobab tree right by my house that we used to attack. Its been there over 50 years. Ohh my how will I sleep tonight. Walahi am dareriin right now.

DALAHOW said...

Hey, that was great..

Mazee when was you last time ulifika kenya...nowadays, Machokoraa wanavaa unii..mats zote zimepigishwa colour na michuki ana rattle watu jo...

ati hata kuna mlendo ati ni chief wa easich...

hee...

KBS is no more..

ma antenooo wengi wamerudi

Anonymous said...

inshaallah walaalo utaregea nyumbani

http://www.youtube.com/watch?v=QUwnCjg9ZEM

Unknown said...

wow....sikujua ya kwamba wewe ni mswahili